Shirikisho la Soka nchini (TFF) limeingia mkataba wa miaka Mitatu na Nusu na Benki ya CRDB kwa ajili ya udhamini wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara.

Mkataba huo wenye thamani ya Bilioni 3.759 umesainiwa leo Jumanne (Aprili 2) katika makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Dar es salaam.

Udhamini huo unaanza rasmi Msimu huu wa 2023/24, ambapo Benki ya CRDB itatoa milioni 255 na udhamini huo katika kipindi cha msimu kilichosalia, ikianza na hatua ya hatua ya 16 bora.

Akizungumzia udhamini huo wa Benki ya CRDB kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’, Wallace Karia amesema: “Benki ya CRDB inakuwa mdhamini wa kwanza wa kombe la Shirikisho Tanzania Bara.”

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema: “Michuano hii sasa itaitwa CRDB Bank Federation Cup, nyote mnafahamu kuwa kwa sasa michuano hii imefikia hatua ya 16 Bora na udhamini wetu unaanza rasmi leo.”

“Kwa misimu mitatu ijayo, Michuano hii itaendeshwa rasmi chini ya udhamini wa Benki yetu ya CRDB,”

“Fedha za udhamini tutakazozitoa zinajumuisha zawadi kwa bingwa wa michuano, mchezaji bora wa kila mechi, mchezaji bora wa mzunguuko, goli bora la mechi, goli bora la mzunguuko pamoja na timu bora ya msimu.” amesema

MALIMWENGU: Masikini anapokula jeuri jeuri yake
Butondo aibana Serikali ujenzi wa Mahakama Kishapu