Rais Samia Suluhu Hassan amezindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mifumo ya Usajili na Malalamiko ya Ukiukwaji wa Misingi ya Ulinzi wa taarifa binafsi na kusema kila Mwanadamu ana utashi na kustahili staha, hivyo zipo baadhi ya taarifa ambazo angependa zisijulikane kwa kila mtu.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo April 3, 2024 Jijini Dar es salaam na kusisitiza kuwa kila Binadamu ana utashi na ana stahili staha, hivyo zipo baadhi ya taarifa ambazo angependa zisijulikane kwa kila mtu kwani ingekuwa hivyo watu wasingetazamana usoni na ndio maana imeanzishwa sheria na Tume ya kulinda faragha za Watu.

Amesema, “miaka ya nyuma ingawa sio nyuma sana huko Duniani kuna visa vilitokea vinavyohusisha kuvuja kwa taarifa binafsi, mifano ya taarifa zinazochukuliwa na Hoteli au Hospitali kuhusu Wateja kuvuja na kuleta athari kwa Wahusika, kuna mifumo ya Kampuni binafsi kutafuta taarifa binafsi za Watu kinyume cha haki za Watu.”

“Haya yote yalisababishwa na udhibiti hafifu wa mifumo ya ukusanyaji, utunzaji na utumiaji wa taarifa binafsi katika Taasisi mbalimbali zilizokusanya na kutumia taarifa binafsi, katika kukabiliana na haya yote ndio maana tupo hapa leo kuzindua Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambapo Katiba ya Tanzania imeweka bayana kulindwa kwa haki za Binadamu ikiwemo kulindwa haki ya faragha,” alisema Rais Samia.

Aidha, amesema, ““Licha ya uwezekano wa taarifa binafsi kutumika kwa hujuma, lakini pia taarifa binafsi ni biashara kubwa kwa makampuni mbalimbali ya kimtandao. Kwahiyo, hatuna budi kulindana ili tusitumike hivyo. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka bayana kulindwa kwa taarifa binafsi za watu au kulindwa kwa haki za binadamu, lakini miongoni mwa haki za binadamu ni kulindwa kwa haki ya faragha.”

Wachezaji Coastal Union warudishwa darasani
Alexander isak kupigwa pini Newcastle Utd