Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imetumia shilingi trilioni 10.69 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha kimataifa yenye urefu wa kilometa 1,219 kuanzia Dar es Saalam hadi Mwanza.

Akielezea utekelezaji wa miradi nane ya kielelezo kwa mwaka 2023/2024 Bungeni leo (Jumatano, Aprili 3, 2024), Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Februari 2024, ujenzi wa reli hiyo umefikia viwango vya kati ya asilimia 5.38 na asilimia 98.84, tayari reli hiyo imeshaanza kufanyiwa majaribio kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Kama nyote mlivyoshuhudia, majaribio ya treni hiyo ya mwendo kasi yalifanyika kwa mafanikio makubwa mwezi Februari, 2024. Ni matarajio yetu kuwa huduma ya usafiri na usafirishaji itaanza ifikapo Julai, 2024 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma,” amesema Waziri Mkuu wakati akiwasilisha Taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2023/2024 na Mwelekeo wa Kazi zake kwa mwaka 2024/2025.

Akifafanua kuhusu ujenzi wa reli hiyo, Waziri Mkuu amesema: “Ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (52.69, Makutupora – Tabora (Kilomita 371) umefikia asilimia 13.86, Tabora – Isaka (Kilomita 165) umefikia asilimia 5.38 na Tabora – Kigoma (Kilomita 506) umefikia asilimia 1.81 Kilomita 300) umefikia asilimia 98.84, Morogoro – Makutupora (Kilomita 422) umefikia asilimia 96.35, Mwanza – Isaka (Kilomita 341) umefikia asilimia.”

Kuhusu mradi wa kuzalisha umeme wa wa Julius Nyerere ambao unatarajiwa kuzalisha megawati 2,115, Waziri Mkuu amesema utekelezaji wake umefikia asilimia 96.81 na kwamba kazi zote za mradi huo zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba, 2024 na kwamba zoezi la kuwasha mtambo wa kuzalisha umeme lilifanyika na kufanikiwa kuingiza kwenye Gridi ya Taifa megawati 235 kutoka kwenye mtambo mmoja kati ya mitambo tisa itakayozalisha umeme katika mradi huo.

Julio kusaka ushindi mwingine Singida FG
Waziri Mkuu: Mapato ya ndani yafikia Trilioni 17