Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile amelazimika kufanya ziara kwa kumtumia usafiri wa Helkopta ya JWTZ kufanya ukaguzi maeneo yote ya Reli ya TAZARA katika eneo la Mlimba Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro ambayo yameharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mara baada ya kufanya ukaguzi huo, Kihenzile amewataka TAZARA kuhakikisha wanafanya haraka iwezekanavyo kutengeneza maeneo yote ambayo yameharibiwa, ili huduma hiyo iweze kurejea.
Amesema usiku wa Machi 31 mwaka huu ilitokea changamoto ya treni kushindwa kuendelea na safari Katika Kijiji cha Lumumwe kata ya Kamwene Halmshauri ya Mlimba Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro baada ya udongo kufunika Reli jambo ambalo lilisababisha abiria zaidi ya 500 kukwama kwa zaidi ya saa 20 katika eneo hilo.
Serikali ilitoa kikosi cha uokozi kutoka JWTZ, ili kusaidia ambao walikua wanatokea Makambako Kuelekea Dar es Salam na tayari zoezi la uokozi limekamilika na kilichobaki matengenezo ya Miundombinu hiyo.