Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Zainab Katimba amesema katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imepanga kutumia jumla ya Sh Bilioni 1.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa km 77.94 na ujenzi wa mitaro yenye jumla ya km 6.395.
Katimba ameyasema hayo hii leo Aprili 5, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu aliyehoji ni upi mpango wa Serikali wa kujenga barabara na mitaro katika Jimbo hilo.
Amesema, “Geita ni miongoni mwa miji 45 inayotekeleza mradi wa Kuboresha Miundombinu Shindanishi katika Miji Tanzania (TACTIC) ambapo mradi utajenga km 17 barabara kwa kiwango cha lami na km 25 za mitaro kwa gharama ya Sh Bilioni 22.23.

Zahera apaza sauti Namungo FC
Kihenzile ahimiza ukarabati TAZARA, ataka huduma zirejee