Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Wafanyakazi Mkoani Manyara wameiomba Serikali kutatua changamoto ya mfumo mpya wa malipo ya mishahara kwa watumishi serikalini wa PEPMIS na PIPMIS ambao umepelekea baadhi ya watumishi kukosa mshahara wa mwezi Machi kutokana na changamoto ya mfumo huo.

Hayo yameelezwa na katibu wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Manyara, Juma David Makanyaga wakati akiwasilisha lisala kwa Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Mei Mosi ambayo kimkoa imeadhimishwa Machi 29 -2024 katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa mjini Babati.

Amesema, mfumo huo mpya wa malipo umekuwa na changamoto kubwa kwa watumishi ambapo umekuwa ukipelekea kuchelewesha malipo ya watumishi hivyo kuiomba serikali kuliangalia suala hilo kwani limekuwa likiwaumiza katika kupata malipo yao kutokana na mfumo huo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Jacob Twange akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameiomba ofisi ya katibu tawala mkoa wa Manyara kushugulikia changamoto hiyo haraka iwezekanavyo ili wafanyakazi waweze kupata stahiki zao kwa wakati.

Awali, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mati super Brand’s ya Manyara,  David Mulokozi amewataka waajiri wenzake wa makampuni binafsi mkoani humo kuwalipa watumishi stahiki zao ikiwemo mishahara kwa wakati pamoja na kuwapa mikataba ya ajira.

Kauli mbinu ya mei mosi mwaka 2024 “Nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao Bora na Kinga dhidi ya Hali ngumu ya maisha.

Bayern Munich kuitega Manchester City
Sheikh Mkuu awaombea mema waathiriwa wa mafuriko