Ili mtoto aweze kumudu maisha yake ya baadaye, mitaala ya elimu haina budi kuangaliwa na kuundwa upya ikiwemo kuweka somo la kumfundisha mtoto namna ya kuitafuta hela, badala ya kumzoesha kuomba.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba katika moja ya mahojiano yake na Dar24 Media na kusema hakuna ubaya kumfundisha mtoto namna ya kutafuta kitu ikiwemo pesa.

Amesema, “endapo ningepata nafasi ya kuongoza sekta ya elimu ningeshauri kufumua mitaala na kuweka somo la utafutaji pesa, hii itamsaidia mtoto kujua matumizi na kuhifadhi akiba, ili aweze kumudu hali ya uchumi na kujiendeleza kimaisha.”

Mbunge wa Jimbo la Kahama, Jumanne Kishimba.

Amesema, ni muhimu kuweka bidii ya kuwafundisha watoto umuhimu na uhalisia wa maisha yaliyopo mtaani, kwani wengi wao wamekuwa wakikosa ajira na hivyo kujikuta na wakati mgumu pale wanapotaka kujiingizia kipato kwa kile walichojifunza shuleni.

“Maana yake hata ukikataa kumfundisha asbuhi atakuomba hela ya Soda, je ukimfundisha yeye kutafuta hela ya soda kutakuwa na ubaya gani, je akijua hela madhara yake huwa nini, atakuwa tu mfanyabiashara na atatunza hela ndiyo ‘logic’ yake,” amesema Kishimba.

Mwanza: Zaidi ya Watumishi 150 washiriki mafunzo mfumo wa NeST
Wairan waandamana kuomboleza kifo cha Raisi