Mbunge wa Rufiji na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ameshiriki utoaji wa misaada ya chakula na malazi kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea katika Wilaya ya Rufiji.

Mchengerwa akiwa na Uongozi wa CCM Mkoa wa Pwani pamoja na Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Mehmet Gulluoglu wametoa misaada hiyo kwa wakazi wa Mohoro walioathirika na mafuriko ambao wamejihifadhiwa katika Shule ya msingi Mohoro.

Amesema, “tunatambua athari zilizoletwa na mafuriko haya kaya nyingi zimeathirika nilikwishatoa Sh.Milioni 40 kwa ajili ya ununuzi wa mbegu kwa wananchi walioathiriwa mashamba yao na mvua lakini kama hiyo haitoshi rafiki zangu wameniunga mkono na sasa tumeleta vyakula pamoja na magodoro kwa kaya zinazoishi katika shule hii.”

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao ametoa rai kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kuhakikisha anasimamia vyema misaada hiyo kwa kuweka mpango wa kuhakikisha wale wenye uhitaji zaidi ndio wanaopata na sio wale wenye kuhitaji nyongeza.

Kwa upande wake, Balozi wa Uturuki nchini, Dkt. Mehmet Gulluoglu amesema wameguswa na adha hiyo iliyowapata wananchi wa Rufiji na ametoa msaada wa vyakula na bahasha ya pole kwa familia zilizothirika zaidi.

Dkt. Mwinyi: Tekelezeni wajibu wenu kwa uadilifu
Tanzia: Malu Stonch wa FM Academia afariki dunia