Mwimbaji nyota wa FM Academia, Emery Malu Stonch amefariki dunia ikiwa ni muda mchache baada ya kuanguka ghafla jukwaani akiimba katika onesho la Bendi hiyo.

Emery Malu Stonch

Malu Stonch alianguka na kupoteza fahamu wakati alipokuwa akiwajibika katika ukumbi wa Target uliopo Mbezi, Beach, jijiji Dar es Salaam usiku wa Jumamosi Aprili 7, 2024.

Malu Stonch (kushoto) na Partcho Mwamba (katikati), wakiimba katika moja ya onesho la bendi ya FM Academia jijini Dar es Salaam.

Taarifa za wadau zinasema baada ya kupatiwa huduma ya kwanza akakimbizwa Hospitali ya Masana ambapo alihamishiwa Lugalo ambapo ilithibitika kuwa tayari alikwisha fariki.

MAFURIKO: Misaada ya kibinadamu yatolewa Rufiji
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 7, 2024