Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi – ACP, Lucas Mwakatundu amethibitisha kukamatwa kwa raia 17 wa Ethiopia katika Kijiji cha Kiongozi, Kata ya Maisaka, Tarafa na Wilaya ya Babati, kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Amesema, Wahamiaji hao, walikuwa wakisafirishwa kwenye gari aina ya V8 VXR yenye namba za usajili STL 1964 huku akiwataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi pale wanapoona watu wasiowafahamu na wenye viashiria vua uhalifu.

Polisi afyatua risasi kukwepa deni la Pombe
Coastal Unoin yakanusha kumtega Ouma