Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta amemwagia sifa mshambuliaji wake Kai Havertz baada ya kuiongoza timu hiyo na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brighton juzi Jumamosi (Aprili 06).

Havertz amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha washika bunduki hao wanaowania kushinda ubingwa wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya England msimu huu baada miaka 20.

Kwenye mchezo huo nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani alionesha kiwango bora na kufunga bao moja kati ya matatu na kuwa mmoja wa wachezaji kwenye kikosi cha timu hiyo wanaozungumzwa zaidi barani Ulaya hasa ikichukuliwa alianza msimu vibaya.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea ilimchukua mechi 10 tangu avae uzi wa Arsenal kufunga bao lake la kwanza kwenye timu hiyo.

Havertz alifunga bao la pili kwenye mchezo huo na sasa ameifungia Arsenal jumla ya mabao 10 kwenye mashindano yote.

“Hakika amekuwa akitoa mchango mkubwa kwenye timu. Kiwango chake kwa ujumla na sasa idadi ya mabao aliyofunga inaongozeka,” alisema Arteta akimzungumzia mchezaji huyo.

“Nafikiri uelewano wake na wachezaji wenzake kwenye ushambuliaji umekuwa mzuri. Nadhani wana muunganiko mzuri, usahihi kwenye kushambulia na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga,” alisema.

Havertz alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo dhidi ya Brighton, tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa msimu wakati mashabiki wengi wa Arsenal walipokuwa wakilalamika kutoelewa nafasi hasa ya mchezaji huyo kwenye timu hiyo.

Joao Felix akoleza usajili wa Silva
Benchikha kuifumua Simba SC 2024/25