Joao Felix amefichua kuwa mchezaji mwenzake wa Ureno, Bernardo Silva ameonesha nia ya kutaka kusajiliwa FC Barcelona.

Huku kukiwa na tetesi za uhamisho zinazomhusisha Silva na uwezekano wa kuhamia Katalunya, uidhinishaji wa Felix unaongeza uzito mkubwa katika hali hiyo.

Ripoti kutoka Hispania zimedai kuwa Silva ana nia ya kutaka kujiunga na Barca, na hivyo kuchochea tetesi kali zinazomhusu nyota huyo wa Ureno.

Felix alisema angependa Silva ajiunge naye Barcelona na wawili hao wamezungumza kuhusu matarajio kama hayo.

“Kama ningekuwa Deco (Mkurugenzi wa Michezo wa Barcelona), ningemsajili Bernardo Silva bila shaka,” alisema Felix.

“Acha wamlete, Umemuona akicheza? Ni bora zaidi kama mtu anatoka kizazi cha Joao Cancelo. Sasa wachezaji wanadumu hadi wana miaka 35 mpaka 36.

“Shemeji yake yuko hapa. aliniuliza kuhusu jinsi mambo yalivyo hapa, hali ya hewa, masuala ya kodi nilimwambia ni sawa kwake kuja.

“Sidhani kama Manchester City itafanya iwe rahisi.”

Felix pia alifichua kwamba Silva angetamani kuvaa jezi ya kifahari akiwa Barca, jezi iliyowahi kupambwa na gwiji wa klabu hiyo, Lionel Messi

“Angependa kuvaa namba 10,” aliongeza Felix

“Ni namba muhimu sana kwenye klabu, huwezi kumpa mtu yeyote tu, Unapaswa kuwa makini. Ni namba ninayoipenda sana, lakini sijawahi kuivaa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 9, 2024
Mikel Arteta amfurahia Kai Havertz