Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali inatarajia kutoa taarifa ya tathmini ya
mazingira hivi karibuni kubaini maeneo yanayokabiliwa na changamoto za mazingira.

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mwera, Zahor Mohammed Haji aliyetaka kujua kuhusu Serikali kuelimisha wananchi
kujiepusha na madhara yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabianchi hadi pale maafa yanapotokea.

Amesema, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa kuelimisha wananchi kuhusu madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi ili waweze kujilinda na maafa na kutaja baadhi ya hatua hizo kuwa ni pamoja na kutoa elimu kupitia njia mbalimbali hasa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Mheshimiwa Naibu Spika, elimu inayotolewa inalenga kukuza uelewa kwa makundi mbalimbali katika jamii hasa wakulima, wavuvi, na wafugaji kuhusu mbinu bora za kilimo, ufugaji na uvuvi endelevu zinazoweza kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi lakini pia kujilinda na maafa yanayoweza kutokea kwa jamii,” amesema.

Katika hatua nyingine, Dkt. Jafo ametoa wito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuangalia namna ya kuvisaidia vikundi vya uzalishaji wa miche ili viwezeze kuzalisha kwa wingi huku, wito alioutoa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Lulindi, Issa Mchungahela aliyetaka kujua hatua ya serikali ya kujengea uwezo vikundi vinahamasisha mazingira.

Gamondi aionya Young Africans Kombe la Shirikisho
Mashujaa kuipima Simba SC kombe la shirikisho