Swaum Katambo – Katavi.
Waislam Mkoani Katavi, wameaswa kuitumia sikukuu ya Eid el fitri kufanya mambo yaliyo mema ya si kufanya mambo ya kumuasi Mwenyezi Mungu kwa kuwa siku hiyo ni siku tukufu.
Wito huo, umetolewa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mashaka Kakulukulu wakati akihutubia ibada ya Sikukuu ya Eid el fitri na kusema kufanya matendo mabaya siku ya Eid ni sawa na kumuasi Mwenyezi Mungu.
Amesema, “siku ya leo atakayefanya madhambi au kumuasi Mwenyezi Mungu ni sawa na mtu ambaye siku ya ufufuo, siku ambayo watu wamefufuliwa mbele ya Mwenyezi Mungu wanasubiria hukumu akaamua kumuasi mbele yake.”