Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka waumini wa dini ya kiislam kuendelea kuyaishi yale waliyojifunza wakati Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ili jamii iendelee kuwa bora na kulifanya Taifa kuwa lenye tulivu, amani na mshikamano.

Majaliwa ametoa wito huo wakati akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu katika msikiti wa Gadaffi jijini Dodoma na kusema kila mmoja anapaswa kufuata misingi iliyoimarishwa kwenye jamii zetu ikiwemo kupinga na kukataa ukatili dhidi ya watoto.

Amesema, “Viongozi wetu wa dini Mwenyezi Mungu amewapa uwezo wa kuhudumia wanajamii na kuwaeleza yaliyomema, na wameendelea kutoa mchango kwenye Taifa hili ili liendelee kuwa na amani, Mwezi huu tumeona utulivu mkubwa, Mimi niwasihi utulivu huutuendelee nao katika kipindi chote cha miezi kumi na moja iliyobaki mpaka kufikia mwezi Mtukufu mwingine.”

Majaliwa amesema, Rais Dkt. Samia amekuwa mfano wa kuigwa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kushiriki ibada ya futari na makundi mbalimbali katika jamii ambayo itawezesha kuijenga jamii yenye misingi imara.

Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka watanzania waendelee kuliombe Taifa ili liendelee kuwa na utulivu na amani akisema, “utulivu wenu Watanzania ndio mmefanya nchi hii iendelee kujiamini na kufanya kazi masaa yote bila shida, huu ndio utamaduni mzuri, tuendelee nao.”

AFYA: Vyakula muhimu katika wa msimu wa joto
Utupaji hovyo chupa za plastiki waundiwa mkakati