Serikali na wadau imeweka mkakati wa kuhakikisha chupa za plastiki za Maji na vinywaji hazitupwi ovyo na kuzagaa, hali inayochangia uchafuzi wa Mazingira.

Hayo yamebainika katika kikao kati ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo na Shirika la PETpro Tanzania linalosimamia urejelezaji wa chupa za plastiki.

Katika mazungumzo na Mratibu Mkazi wa shirika hilo, Nicholaus Ambwene aliyeambatana na Mchambuzi Oliva Gabriel, Dkt. Jafo
amesema Serikali inatarajia kuwashirikisha wazalishaji wa chupa za plastiki kuhakikisha urejelezaji unafanyika inavyotakiwa.

Amesema tatizo la kuzagaa kwa chupa za plastiki limekuwa kubwa hivyo ipo haja ya kuwashirikisha wadau wa uzalishaji wa chupa hizo
zinazotumuka kuhifadhia maji na vinywaji katika kuhakikisha changamoto hiyo inamalizika.

Awali, Ambwene aliwasilisha mrejesho wa shughuli zinazofanywa na PETpro tangu kuanzishwa kwake, maoni, changamoto na mikakakati endelevu.

Majaliwa: Endeleeni kuyaishi ya mwezi Mtukufu
Vyombo vya Habari kutotangaza, kuchapisha habari za siasa