Kufuatia kusitishwa kwa shughuli za vyama vya siasa, Mamlaka Kuu ya Mawasiliano Nchini Mali – HAC, imevitaka Vyombo vyote vya Habari kusitisha utangazaji na uchapishaji wa shughuli zote za vyama vya siasa.

Hatua hiyo, inatokana na tangazo la utawala wa kijeshi la Aprili 10, 2024 kuagiza kusitishwa kwa shuguli zote za kisiasa hadi uamuzi mwingine utapotolewa baada ya tamko la pamoja la vyama vya siasa zaidi ya 80 kutaka uchaguzi wa kiraia haraka.

Kiongozi wa Kijeshi wa Mali, Kanali Assimi Goita.

Katazo hilo linakuja wakati jeshi limeshindwa katika ahadi yake, iliyotolewa chini ya shinikizo la Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), kukabidhi madaraka kwa raia ifikapo Machi 26, 2024.

Taifa hilo la Afrika magharibi limeongozwa na wanajeshi tangu mapinduzi ya mfululizo mwaka 2020 na 2021, huku hali ya usalama pamoja na mzozo wa kisiasa na kibinadamu ikizidi kuwa mbaya.

 

Utupaji hovyo chupa za plastiki waundiwa mkakati
Mafuriko Rufiji, Kibiti: Ulega akabidhi Boti, Chakula