Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho hakitaki uongozi wa kuwagawanya watu kwakuwa unapeleka mpasuko na kukwamisha maendeleo.
Nchimbi ameyasema hayo hii leo Aprili 13, 2024 katika ziara yake Mkoani Katavi na kuongeza kuwa moja ya changamoto kubwa iliyopo ndani ya CCM ni tabia ya baadhi ya viongozi wanaoshindwa na wanaoshinda kutokukubali matokeo miyoyoni mwao.
Amesema, “Chama cha Mapinduzi hakitaki na kinakemea tabia ya Uongozi wa kugwanya watu kwakuwa unapelekea mpasuko ndani ya Chama na kukwamisha maendeleo kwa Watanzana. ”
Amebainisha kuwa, “moja ya changamoto kubwa iliyopo ndani ya CCM ni tabia ya baadhi ya viongozi wanaoshindwa na wanaoshinda kutokukubali matokeo miyoyoni mwaona matokeo yake pamoja na uchache wao lakini wanakuwa na madhara makubwa na kusema tabia hiyo iachwe mara moja kwakuwa ni ujinga na sio misingi ya demokrasia.”
“Unakuta mtu kagombea na kashida lakini akimaliza kushinda anaanza kutafuta nani hakumuunga mkojo ili apambane nae na kumkandamiza, hiyo ni tabia ya kijinga na haiungwi mkono, tuache mara moja,” alisema Balozi Dkt. Nchimbi.
Aidha, alihimiza juu ya misingi ya haki na wajibu na kusema mtu yeyote anapoingia kwenye uchaguzi anatakiwa kufahamu kila mtu ana haki sawa na mwengine hivyo ni lazia uwe na dhamira ya utumishi na wakati mwingine usipochaguliwa unatakiwa kuhisi kwamba mzigo mkubwa umekuepukia.
“Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ‘Mimi nanga’atuka lakini naendelea kuamini kuwa bila CCM madhubuti nchi hii itayumba’ hivyo niwaambie ndugu zangu mtu asiyeitakia mema nchi hii atatamani kuona CCM inapasuka,” alisema.
Hata hivyo, Nchimi amsema, “tujue kwamba CCM madhubuti inaongozwa na misingi ya demokrasia na kiongozi wa kweli ni yule ambaye anakubali matokeo bila vita, mimi nilishawahi kugombea mara 28 na mara 4 nilishindwa lakini naelewa kuna kushinda na kushindwa na matokeo nikakubali.”