Jumla ya Shilingi Milioni 132 zimekusanywa na ahadi ya vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 50 ikiwa ni michango ya hali, vifaa, huduma na Wataalamu inayofikia zaidi zaidi ya Shilingi Milioni 400 kutoka kwa Mashirika na Makampuni kwa ajilinya ujenzi wa Shule ya Wavulana ya Bunge.

Akizungumza jijini Dodoma  hii leo Aprili 13, 2024 katika tukio la Bunge Marathon, Spika wa Bunge na Rais wa umoja wa Mabunge Duniani – IPU, Dkt .Tulia Ackson amesema mbio hizo za hisani zimekuwa ni njia mojawapo ya kuleta pamoja juhudi za wadau na taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na Bunge.

Amesema, “nadhani lengo letu limetimia kwa kuwa tulihitaji ushirikiano wa Taasisi mbalimbali za Serikali, Mashirika na makampuni ya Umma na yale ya binafsi, yakiwemo Mabenki, Taasisi za kijamii, Mashirikisho ya Michezo na wadau wa mchezo wa mbio za riadha ili kufikia lengo letu.”

Dkt. Tulia ameongeza kuwa, Bunge limeshiriki katika kutatua changamoto ya kupata elimu, kwa mtoto wa kike, ambapo lilichangisha fedha toka kwa wabunge na kwa wadau wengine, zilizowezesha kujenga shule ya Wasichana ya Bunge, iliyopo eneo la Kikombo, hapa Dodoma.

Shule hiyo ya Wavulana inatarajiwa kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu, kwa kuwa haitatofautiani na ile ya Wasichana kwa maana ya miundombinu yake ambayo itakuwa bora zaidi na yenye uwezo wa kupokea Watoto 600-700.

Uongozi wa kuwagawa watu unaturudisha nyuma - CCM
Dkt. Nchimbi: Hatutasikiliza kero zilizo Mahakamani