Swaum Katambo –  Katavi.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka Viongozi mbalimbali nchini kuwa na utaratibu wa kuwataarifu Wananchi juu ya kazi za maendeleo zinazofanywa na Serikali, ili kupunguza maswali kwa jamii.

Balozi Dkt. Nchimbi ameyasema hayo akiwa katika ziara yake ya kwanza Mkoani Katavi alipokuwa akitoa salam za Chama katika ofisi ya CCM Mkoa, huku akitoa tahadhari ya kutosikiliza kero ambazo zinaendelea Mahakamani.

Dkt. Nchimbi tayari ameanza ziara yake mkoani Katavi ambayo ni sehemu ya ziara hiyo kwa mikoa sita atakayotembelea ikiwemo Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Bunge Marathon yakusanya Mil. 132 za Shule ya Wavulana
Mahakama yataifisha V8, Waethiopia wakubali yaishe