Mahakama ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa, imetaifisha kuwa mali ya Serikali, gari aina ya Toyota LandCruiser V8, lililokamatwa likiwa limebeba Wahamiaji haramu 16 Raia wa Ethiopia April 6 2024 katika eneo la Msitu wa Luganga kata ya Sao Hill.

Aidha, uamuzi huo umeenda sambamba na raia hao 16 wa Ethiopia kuhukumiwa adhabu ya kulipa faini ya Shilingi 500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Akitoa huku hiyo, Hakimu Mkazi wa Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Benedict Nkomola aliwatia hatiani baada ya washitakiwa kukiri makosa, huku wakishindwa kulipa faini hiyo na kupelekwa gerezani.

Walikamatwa Aprili 6, 2024 na Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wa Maofisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wakisafirishwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 lenye namba za usajili T803 CVW.

Dkt. Nchimbi: Hatutasikiliza kero zilizo Mahakamani
Viongozi wachonganishi wamsikitisha Rais Samia