Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewasihi watanzania kufanya maamuzi sahihi kwa kuchagua viongozi watakaoleta maendeleo kwani Wananchi wanachotaka ni maendeleo na sio siasa wakati wa uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Biteko pia ameagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha linapeleka huduma ya umeme kwenye maeneo ya miradi ya maendeleo ili kuharahisisha huduma kwa wananchi.

Dkt. Biteko amesema hayo akiwa Loliondo, wilayani Ngorongoro baada ya kuzindua minara ya kurushia matangazo na kusema miradi inatekelezwa na itakuwa ya mafankio endapo Taasisi husika zitakaa pamoja na kuandaa maeneo yanayohitaji utekelezaji katika hatua mbalimbali na kwamba TANESCO, REA, UCSAF na TBC zikae pamoja wakati wa uandaaji wa miradi husika ili iwe inatekelezeka kwa tija, ufanisi na kwa haraka.

Pia, ameiagiza TARURA kuhakikisha huduma ya barabara zinafikika katika maeneo ilipojengwa mitambo ya redio ambayo ipo sehemu kubwa ya milimani nchini ili kuwa na miundombinu imara na kuwataka wananchi ambao mitambo hiyo imezinduliwa katika wilaya za Ngorongoro, Arusha, Uvinza Kigoma, Makete – Njombe na Kyela Mbeya, kuhakikisha wanaitunza mitambo hiyo kwa maslahi ya wananchi wote.

 

Gamondi: Simba SC hainipi Presha
Shughuli za uokozi: Ulega amkabidhi Boti Kunenge