Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amepokea Msaada wa boti yenye mashine kutoka kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega, ambaye aliwakilishwa na Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM wilaya ya Mkuranga, Omari Kisatu.

Boti hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 42 itatumika kwa ajili ya shughuli mbalimbali za usafiri na uokozi wa Waathirika wa mafuriko yanayoendelea katika mto Rufiji, kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti Mkoani Pwani, iliyokabidhiwa kwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Jennifer Shirima.

Akikabidhi Boti hiyo, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mkuranga, Omary Kisatu kwa niaba ya Ulega alisema boti hiyo imeletwa kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za maafa yaliyojitokeza kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote.

Naye Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Jennifer Shirima alishukuru kwa msaada huo na kuomba Wadau wasaidie zaidi upatikanaji wa Boti kutokana na mahitaji makubwa kwani zipo boti tatu zinazotumika katika uokoaji.

Dkt. Biteko: Watanzania fanyeni maamuzi sahihi
Ally Kamwe: Msije na matokeo Uwanjani