Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kupitia kwa Mwenyekiti wa Mkoa Kagera, Wales Mashanda amewataka Wakandarasi wa Halmashauri ndani ya Mkoa huo waache tabia ya kujifungia ndani na badala yake wabadilike na kutoka nje, ili wapate mawazo mapya yatakayoweza kuwasaidia kujenga miundombinu na kuboresha miradi mbalimbali ya Serikali.
Ameyasema hayo wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa uzio wa shule ya Mgeza Mseto, ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara wa Shule ya sekondari Kyamigege kata ya Kagondo,Zahanati ya kibeta na kituo cha Afaya kinacho endelea kutoa huduma Zamzam ambapo amesema kuwa kwa sasa kumekuwepo na tabia ya wakandarasi wa Halmashauri kukaa eneo moja jambo ambalo halileti ufani kwenye miradi inayotekelezwa.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Godson Goypson ameshukuru kwa Viongozi hao kwa kutembela na kuiona miradi inayotekelezwa kwa nye Manispaa hiyo ikiwemo kituo cha Afya Zamzam ambacho Serikali imekipatia x-ray mpya ya shilingi milioni 250 na Zahanati ya kibeta iliyogharimu shilingi milioni 100.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Kyerwa, Bahati Enerco amesema ziara hiyo itawasidia kuwaongezea uzoefu katika usimamizi wa miradi inayoendelea kutekelezwa na ushauri wakandarasi kufanya Mawasiliano ili kuwajengea uzoefu.