Baraza la Magavana Nchini Kenya – COG, Nchini Kenya limeionya Serikali kuu kuitaka kutekeleza mkataba wa maelewano, waliowekeana na madaktari mapema mwaka 2017.
Magavana hao, wanasema kutekelezwa kwa mkataba huo wa mwaka 2017/2021, huenda kukaitumbukiza nchi kwenye shida zaidi kwani tayari Madaktari wameshikilia msimamo wao kuwa lazima utekelezwe.

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana, Ann Waiguru amesema huenda Kaunti za Taifa hilo zikaathirika zaidi, kwani itabidi Wafanyakazi wengine wa Serikali waanze kutoa matakwa yao.