Droo ya hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB imekamilika huku vigogo wanane waliofuzu hatua hiyo wakibaini wapinzani wao.

Timu zilizofuzu hatua ya Robo Fainali ni Namungo FC, Geita Gold FC, Tabora United, Coastal Union, Ihefu SC, AzamFC, Mashujaa FC na Young Africans.

Mabingwa watetezi, Young Africans anga SC amekutanishwa na Tabora United huku Wanalambalamba, Azam Fc wakipewa Namungo FC yenye maskani yake Ruangwa.

Wagosi wa Kaya, Coastal Union watakuwa na kibarua dhidi ya wachimba dhahabu, Geita Gold FC wakati Ihefu FC (Sasa Singida Black Stars) wakipewa mfupa uliowashinda Simba SC, Mashujaa FC.

Droo Kamili.

Young Africans Vs Tabora United

Azam FC Vs Namungo FC

Coastal Union Vs Geita Gold FC

Ihefu FC Vs Mashujaa FC

Michezo ya Robo Fainali itachezwa kati Mei 2-4, 2024.

Mshindi kati ya Young Africans na Tabora United atachuana na mshindi kati ya Ihefu FC dhidi ya Mashujaa FC kwenye hatua ya Nusu Fainali.

Mshindi kati ya Azam FC dhidi ya Namungo FC atachuana na mshindi kati ya Coastal Union dhidi ya Geita Gold kwenye Nusu Fainali.

Jemedari afichua ukweli ofa ya Mzize
Mgomo wa Madaktari: Magavana waionya Serikali Kenya