Wakati tetesi zikieleza kuwa Uongozi wa Azam FC umewasilisha ofa kwa mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans ukihitaji huduma ya Mshambuliaji Clement Mzize, Mchambuzi wa Soka Tanzania Jemedari Said Kazumari amefichua baadhi ya mambo kuhusu ofa hiyo.

Azam FC imekuwa ikitajwa kuwasilisha ofa hiyo tangu jana Jumatatu (Aprili 15), ikiamini Mshambuliaji huyo atatosha kuziba pengo la Prince Dube aliyeomba kuvunja Mkataba kabla ya kujiweka pembeni.

Jemedari ametumia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii akikanusha taarifa zinazoambatana na ofa hiyo, ambapo inadaiwa kuwa Azam FC imependekeza dili la usajili wa Mzize lihusishwe na uhamisho wa Price Dube ambaye anatajwa kuwaniwa na Young Africans.

Jemedari ameandika: Jumatatu tarehe 15 April 2024 uongozi wa Azam FC @azamfcofficial ulipeleka ofa kwa klabu ya Yanga SC @yangasc wakitaka kumsajili mshambuliaji kinda wa klabu hiyo Clement Mzize, ofa ya Azam FC ni Ths 400,000,000/= (400M), baada ya kupokea ofa hiyo siku iliyofuata yani Jumanne tarehe 16 April 2024, uongozi wa Yanga ukaijibu barau ya Azam FC kwamba wao kama viongozi watakaa na kujadili ofa hiyo kisha watawajibu.

Kwenye ofa ya Azam FC hakuna sehemu yoyote ambayo imezungumzia suala la kubadilishana wachezaji (swap deal) kati ya Clement Mzize na Prince Dube ambaye yupo kwenye matatizo na Azam FC. Azam FC wamepokea maelekezo ya kocha wao kwamba anataka washabuliaji 2 mmoja mzawa na mwingine mgeni, mzawa anamtaka Mzize. Ndipo vongozi wa Azam FC wakatoka na ofa ya 400M, HAKUNA KUBADILISHANA WACHEZAJI.

Kilichotokea baada ya Azam FC kuweka pesa mezani, Mzize kaingiziwa pesa za kuongeza mkataba na klabu yake ya Yanga ambapo bado wapo kwenye maongezi ya mkataba mpya.

Watu wa karibu yake  wamethinitisha hili na habari zinasema huenda muda wowote Clement Mzize ataongeza mkataba na Mabingwa wa nchi. Kama ana wasimamizi imara manake ni kwamba anaweza kuzoa zaidi ya 400M kutoka Yanga, Kwani Azam wako mlangoni. Ila kwa kariba ya wachezaji wetu utakuja kusikia kituko utaziba uso.

NB: Mzize anahusishwa na kutakiwa na klabu ya Watford ya England, lakini Mzize pia aliwahi kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Marseille ya Ufaransa, akili kichwani mwake na wanaomzunguka.

Waiomba Israel isilipe kisasi, yenyewe yajipanga
Robo Fainali kombe la shirikisho hadharani