Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na wa Uingereza David Cameron, wapo nchini Israel kuelezea wasiwasi wao kuhusu hofu ya mzozo unaoendelea Gaza, ikiwemo kutanuka kuwa mzozo wa kanda nzima iwapo litafanyika shambulio la kulipiza.

Mawaziri hao, Annalena Baerbock alikutana na mwenzake wa Israel, Israel Katz wakati wa ziara yake ya saba, tangu Hamas ilipovamia kusini mwa Israel na pia alikutana na pia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na aliyekuwa mkuu wa upinzani nchini humo Benny Gantz.

Katika mazungumzo yake na viongozi hao, Baerbock alijadili kwa kina hofu ya vita vinayoendelea katika Ukanda wa Gaza, kusambaa katika mataifa mengine na kuwa mzozo mkubwa wa kikanda.

Aprili 13, 2024, Iran ilirusha madroni na makombora nchini Israel kujibu shambulizi linalodaiwa kufanywa na Tel Aviv katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascu, Syria ambapo Israel imeapa kulipiza kisasi, ambapo washirika wa Israel wanawasiwasi huenda kukazuka mgogoro katika eneo la Mashariki ya kati.

Watanzania waombwa AFCON 2027
Jemedari afichua ukweli ofa ya Mzize