Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amewaomba Watanzania kuchangamkia fursa zitakazotokana na kuwa wenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2027’.

Tanzania kwa kushirikiana na nchi jirani za Kenya na Uganda zitakuwa wenyeji wa michuano hiyo mikubwa kuliko yote katika ngazi timu za taifa Barani Afrika mwaka 2027.

Akizungumza katika Kongamano la Uwekezaji kati ya wadau wa sekta ya michezo kujadili fursa kuelekea AFCON 2027, , Msigwa amesema kuna fursa nyingi za kiuchumi zitakazoambatana na Tanzania kuwa wenyeji wa michuano hiyo ambayo Watarzania wanapaswa kuzichangamkia.

“Wawekezaji wa Kitanzania mnapaswa kujisajili na kuanza kutekeleza fursa za miradi ya ujenzi wa hoteli za kisasa na nyumba za kulala wageni zitakazojengwa kwa ajili ya AFCON 2027,” amesema Msigwa.

Amesema sekta binafsi zinapaswa kuwekeza kwenye michezo kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya miundombinu kuelekea mashindano hayo.

“Kuna mahitaji makubwa ya miundombinu ya michezo kuelekea AFCON 2027 ambayo sekta binafsi haina budi kuchangamkia fursa hizo,” amesema Msigwa katika kongamano hilo.

Serikali yaendeleza mikakati kukabili Malaria, Mbu
Waiomba Israel isilipe kisasi, yenyewe yajipanga