Lydia Mollel – Morogoro.
Ubalozi wa Norway Nchini, umesema utaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine cha Morogoro – SUA, katika kufadhili na kutekeleza Miradi mbalimbali ya Kilimo, Ufugaji na mabadiliko ya Tabia ya nchi (Hewa hukaa).
Hayo yamebainishwa na Balozi wa Norway Nchini, Tone Tinnes katika ziara yake Chuoni hapo iliyolenga kutembelea na kukagua Miradi inayotekelezwa na SUA kwa kushirikiana na Norway.
Naye Mkurugenzi wa kitengo cha Taifa cha kuratibu Hewa ukaa, Prof. Eliachim Zahabu amesema uanzishwaji wa kituo hicho kimetokana na ufadhili wa nchi hiyo, hivyo balozi huyo ametembelea kuona kile kinachofanyika kwa sasa na kipi kifanyike baada ya hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Raphael Chibunda amesema ziara hiyo ni moja ya makubaliano ambayo SUA kilisaini na Chuo Kikuu cha Sanyansi Nchini Norway kufuatia ziara ya Rais Samia wamekubaliana kufanya mambo makuu matatu lakini kubwa zaidi ni kushirikiana katika sekta ya Kilimo.