Baada ya kuliweka kabatini taji la 20 la Ligi Kuu ya Italia ‘Sirie A’, Mkurugenzi wa Michezo wa Inter Milan Piero Ausilio ameanza tambo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu  nchini humo na Michuano ya Kimataifa.

Inter Milan ilijihakikishia Ubingwa huo usiku wa kuamkia leo Jumanne (Aprili 23), baada ya kuichapa AC Milan 2-1, na kufikisha alama 83 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Italia ‘Sirie A’, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote inayoshiriki Ligi hiyo msimu huu 2023/24.

Piero Ausilio ametangaza kuwa mabingwa hao wapya tayari wameimarika kwa ajili ya msimu ujao 2024/25, hivyo hawana wasiwasi wa kupambana na kuendelea kuweka heshima ya mataji.

Ausilio amethibitisha uhamisho wa Bosman kwa kiungo wa SSC Napoli Piotr Zielinski na mshambuliaji wa Porto Mehdi Taremi.

Kiongozi huyo amesema: “Huu ni wakati wa wote kufurahi pamoja, tayari tumefanya kitu kidogo na labda haraka sana kwa sababu sasa kila mtu anatarajia zaidi. Lakini tayari tumefanya mambo kadhaa … ni Zielinski na Taremi. ”

Mkurugenzi wa Michezo wa Inter Milan Piero Ausilio

“Tulikuwa tayari tumemtambua (Marcus) Thuram miaka miwili iliyopita, huwa kuna kazi nyingi nyuma yake na ikiwa leo yuko Inter na anafanya anachofanya pia ni kutokana na mipango iliyoanza miaka miwili iliyopita.

Baada ya kusema maneno hayo yenye tambo, Ausilio akafunguka kuhusu maisha yake klabuni hapo, akiwataja baadhi ya viongozi aliowahi kufanya nao kazi na kumpa moyo.

“Kumekuwa na wakati mgumu katika utendaji kazi, nilijiunga na Inter nikiwa mtoto na nilikuwa na nywele chache za ziada. Katika miaka ya hivi karibuni nimepata ushauri mwingi na nimekusanya uzoefu mkubwa na wamiliki watatu tofauti, kisha familia ya Moratti. Alinitambulisha kwa ulimwengu huu, Thohir alikuwa wa kwanza kunipa majukumu fulani na kisha na kundi la Suning likaundwa kundi la ajabu, kuna huruma kubwa kati yetu, kuna tamaa ya kufanya vizuri tu.” amesema Ausilio

SUA, Norway kushirikiana uimarishaji sekta ya Kilimo
Stefano Pioli: Wachezaji wajitume, sifikirii kujiuzulu