Meneja wa AC Milan Stefano Pioli amewahimiza wachezaji wa klabu nyingine za Ligi Kuu ya Italia ‘Sirie A’ kucheza kwa kujituma ili kupunguza pengo dhidi ya mabingwa wapya Inter Milan.

AC Milan walipoteza mchezo dhidi ya Inter kwa mabao 2-1 jana Jumatatu (Aprili 22) huku vijana wa Simone Inzaghi wakitawazwa kuwa mabingwa kwa mara ya 20 wa Ligi Kuu ya Italia ‘Sirie A’.

Inter kwa sasa wapo mbele kwa alama 17 mbele ya AC Milan huku kukiwa na mechi saba za kucheza kabla ya kumalizika kwa msimu huu 2023/24.

Kocha Stefano Pioli amesema pengo liko wazi kati ya timu ya Inzaghi na ligi nyingine, lakini kuna haja kwa wachezaji wa timu nyingie kujituma ili kupunguza pengo hilo, japo Bingwa ameshapatikana.

“Inter walikuwa na kampeni ya kipekee, walipoteza mechi moja tu, lakini kwa miaka mitatu au minne sasa hakuna anayeweza kutilia shaka kuwa wamekuwa na kikosi imara zaidi kwenye ligi,” amesema Pioli

“Kwa upande wetu, tulipoteza pointi katika baadhi ya michezo muhimu na kukosa uthabiti.

“Ikiwa pengo kati ya Inter na timu zingine ni kubwa hivyo, inamaanisha ni timu yenye nguvu sana na sote tunapaswa kuongeza kiwango.”

Kipigo dhidi ya Inter kinaashiria kipindi kigumu kwa AC Milan ambacho pia kiliwafanya waondolewe kwenye Michuano ya Ligi ya Ulaya ‘UEFA Europa League’ dhidi ya AS Roma.

Pioli amesema: “Tulikuwa tukitoka kushinda saba mfululizo, kwa hiyo mechi mbili za Europa League dhidi ya AS Roma hazikuwa kile tulichotaka au tulichotarajia. Tulikuwa na kila mtu katika hali nzuri na kujiamini, lakini tulifanya kazi mbili ambazo zilikuwa chini yetu. viwango.

“Ilitokea Daby kuwa mchezo uliokuwa unafuatia. Nadhani labda ilikuwa daby ya usawa zaidi ya makutano ya hivi karibuni, tulikuwa na bahati mbaya.

“Nilijaribu kuongeza morali ya vijana, kwa kuwa ni kipigo kilichoniuma zaidi kwa kila kitu kilicho nyuma yake. Nilijaribu kadri niwezavyo kuwatuliza wachezaji wangu, kwa sababu tunahitaji kumaliza msimu vizuri, tuna mchezo mwingine muhimu. Jumamosi dhidi ya Juventus inayoshika nafasi ya tatu.

“Kwa bahati mbaya, hatukuweza tena kupata sare katika daby hii.”

Kuondolewa kwa Ligi ya Europa na pengo la alama dhidi ya Inter kumesababisha kuongezeka kwa uvumi kwamba Pioli ataondoka San Siro mwishoni mwa msimu huu, lakini mmoja wa bosi huyo wa AC Milan amesema angependa kuendelea.

“Sijui kama nitaondoka. Inzaghi alionekana kuhangaika miezi 14 iliyopita kwa mujibu wa vyombo vya habari na angalia alichofanikisha baada ya hapo. Nina furaha hapa, ninafanya kazi vizuri na nadhani timu ina nafasi ya kuboresha. Tutaona tulipo sote mwishoni mwa msimu na tujadili.” amesema Kocha huyo

Piero Ausilio: Inter Milan tupo tayari kwa 2024/25
Simone Inzaghi: Haikuwa rahisi, lakini imewezekana