Wakati Serikali Nchini Kenya ikiunda kikosi cha dharura kushughulikia janga la mafuriko, miili ya watu takribani 13 imeopolewa kutoka maeneo tofauti ya mji mkuu wa Nairobi, huku Polisi wakiendelea na juhudi za uokoaji.

Hali hiyo, imetokea kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha, huku ikiarifiwa kuwa miili 11 imepatikana eneo la Mathare, mmoja Kibera na mingine mtaani Kayole, mitaa ambayo imejengwa kwa mabanda huku ikihofiwa kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Hata hivyo, mvua hizo zimewaacha mamia ya watu bila makazi kwani mvua hiyo imesababisha mafuriko yaliyoathiri nyumba na baadhi ya barabara ambazo kwasasa hazipitiki kutokana na kuharibika na zingine kujaa maji.

Mkuu wa Polisi kaunti ya Nairobi, Adamson Bungei amesema zoezi la uokozi linaendelea kwa kushirikiana na vikosi vya idara mbailimbali kutoa usaidizi huku wakaazi wa maeneo yaliyo kwenye kingo za mito wakishauriwa kuhama.

Zidane aonywa kuichukua Bayern Munich
TPBRC yateuwa Kamati ya Rufaa