Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Lazarus Kambole ameiweka pabaya Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2023/24, ambapo Klabu za soka Tanzania zitafanya usajili kuelekea msimu ujao 2024/25.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema leo Jumanne (Aprili 30) na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ na kusainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shiriukisho hilo Cliford Mario Ndimbo imeeleza kuwa, Young Africans imefungiwa kufanya usajili huku Kambole akitajwa.

Maamuzi hayo yametolewa baada ya Mshambuliaji huyo kuishtaki Young Africans kwenye Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba.

Young Africans ilitakiwa iwe imemlipa Kambole ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Taarifa hiyo ya TFF imeeleza: Klabu ya Young Africans iliyoko Ligi Kuu ya NBC, imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa aliyekuwa mchezaji wake Lazarus Kambole.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya kiabu hiyo.

Mchezaji huyo raia wa Zambia alifungua kesi FIFA akidai malipo ya malimbikizo ya mishahara na fidia ya kuvunjiwa mkataba.

Young Africans ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo.

Wakati FIFA imeifungia kiabu hiyo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.

TFF inazikumbusha kiabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha iii kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.

Mgunda kuanza Simba SC bila wachezaji sita
Wachezaji Chelsea wampambania kocha