Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wakandarasi wazawa waliopewa dhamana ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliji kuhakikisha waaitekelza kwa weledi na ubora.
Majaliwa Ameyasema hayo katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa Miradi ya umwagiliaji katika maeneo mbalimbali, iliyofanyika jijini Dodoma.
Amesema, “ndugu washiriki nimefurahishwa kuona kuwa asilimia 82 ya wanaokwenda kujenga miradi hii ni wataalamu na hizi ni fursa za ajira kwa Watanzania, lakini ni fursa ya kuongeza ujuzi kupitia miradi hii, vilevile inakwenda kuongeza kipato kwa Watanzania.
Aidha Waziri Mkuu pia aliongeza kuwa, “nitoke rai kwa wakandarasi wazawa, kwanza mbadilike, mnathaani kubwa mmepewa ya kutekeleza miradi na hili ndicho kilio kikubwa cha private seckta (sekta binafsi) leo mmeona serikali imeendelea kutekeleza kwa kuwapa miradi.”