Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao maeneo yao kuna misitu ya asili kuhakikisha wanaanzisha biashara ya hewa ukaa kama chanzo kipya cha mapato.

Mchengerwa ameyasema hayo wakati akifunga kikao cha siku tatu na Wakurugenzi hao kilichofanyika shule ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo kibaha mkoani Pwanina kudai kuwa biashara ya kaboni ni biashara mpya na inafanya vizuri sana kwenye baadhi ya Halmashauri kama vile Tanganyika na ni chanzo kizuri cha mapato na cha uhakika.

Amesema, “Halmashauri zingine zote zenye misitu zinatakiwa kuanza biashara hii mara moja, ninawapa mwezi mmoja Halmashauri zote zenye Misitu muende mkajifunze kwa Halmashauri ya Tanganyika ambao wameshafika mbali kwenye Biashara hii na kwa mwaka wanapata Sh. Bilioni 14 ambazo zinasaidia kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kuongeza mapato ya Halmashauri.”

Mchengerwa ameongeza kuwa, “mtakumbuka kuwa wiki mbili zilizopita wakati nafungua Mkutano wa 38 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania niliwaelekeza kila Mkurugenzi kuhakikisha ameanzisha vyanzo vipya viwili vya mapato sasa niwape chanzo cha kuanza nacho ni hiki cha hewa ukaa,”amesema.

Mrithi wa Lomalisa yuko njia panda
Kocha Kitambi aitambia Namungo FC