Eva Godwin – Dodoma.

Katika kuangalia uwezekano wa matumizi ya akili bandia kufanya mapitio ya matumizi ya umma, Serikali imefanya mazungumzo na Wataalam kutoka Oxford Policy Management.

Mazungumzo hayo, yamefanyika ya Wataalamu hao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi ofisini kwake Jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi amesema pia lengo la mazungumzo hayo ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto nchini. kufuatia Serikali ya Tanzania kuzindua Programu ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM), mwaka 2021.

Uzinduuzi huo ni mpango mkuu wa kuzileta pamoja Wizara na wadau mbalimbali, ili kuboresha makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 8.

MALIMWENGU: Ukiona ya njege ni kama njigi
Magendo: Madiwani waivuta shati Kamati ya usalama