Kinachoshangaza ni utamaduni waliojiwekea Binadamu kulingana na maeneo wanayoishi, ambao wengine hufanya ni kanuni kuu zinazotakiwa kufuatwa na kila mtu ili aweze kuzitii kulingana na utaratibu wa ukoo, jamii, kabila au kikundi fulani chenye mwongozo.
Wapo ambao hutumia sauti zenye toni mbalimbali katika kukubali au kukataa jambo ambapo pia hutumia ishara kutikisa sehemu ya mwili kuonesha au kuelekeza kitu au jambo pale anapoulizwa swali, lakini cha kushangaza kuna baadhi ya maeneo huwa ni tofauti.
Mfano kwa hapa kwetu huwa tunatumia sana kidole au mkono na imezoeleka sana kwa kabila mbalimbali au tuseme maeneo mengi ni hivyo Duniani lakini si katika Taifa la Nicaragua, kwani wao huonesha ishara kwa kutumia midomo badala ya kidole kama watu wengi walivyozoea duniani.
Midomo inatumika kwa ishara ya kukubaliana kitu, kuonyesha kitu ama njia ya kukupa ujumbe, hivyo basi unatakiwa kuwa makini sana pale unapokuwa kwenye mazungumzo na Mnicaragua kwa kumtazama na kumfuatilia kwa ukaribu kwenye midomo yake kuweza kumuelewa usisubiri mikono yake utafeli.
Waweza kustaajabia lakini nikuhakikishie tu kwamba wenyewe wanaelewana vizuri na ni kitu kinachowatambulisha kwa ukaribu katika kijamii yao hivyo kama utabahatika kwende katika Nchi hiyo uwe umejipanga na ukirudi pia kumbuka sisi tunatumia mkono au Vidole hivyo usichanganye mambo.