Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amekiri wazi kuvutiwa na uwezo wa Kaimu Kocha Mkuu wa kikosi chao Juma Ramadhan Mgunda, lakini ameuachia uongozi wa Klabu hiyo kufanya maamuzi.
SImba SC kwa sasa ipo kwenye mchakzto wa kumsaka mrithi wa Abdelhak Benchikha aliondoka klabuni hapo na kurejea nchini kwao kwa sababu za kifamilia, huku Mashabiki na Wanachama wengi wakishinikiza timu yao ikabidhiwe rasmi kwa Juma Mgunda.
Ahmed amesema Kocha Mgunda amedhihirisha kuwa na ubora wa kuifundisha Simba SC, ambayo ilionekana kuwa hohe hahe, lakini baada ya kukabidhiwa kwa kocha huyo mzawa imekuwa na matokeo mazuri.
“Kwa kweli Juma Mgunda ni Kocha mzuri sana, hebu fikiria unamkabidhi timu kocha huyu akiwa na mshambuliaji tegemeo kutokea pembeni kama Chasambi, akiwa na mshambuliaji tegemeo kutokea pembeni kama Balua na akiwa na beki wa pembeni kama Israel Mwenda, bado amefanya kazi na hawa watu na Simba SC inapata matokeo mazuri, unadhani nini ni kimeleta hii kitu? Ni ubora aliokuwa nao Mgunda.
Kwanza ameshatwaa Ubingwa kwenye Ligi Kuu ya Wanawake, taarifa sijui mnazo? Jana tumeshinda mabao manne, huyu ni Kocha Bora sana, kwa sababu ndani ya msimu mmoja amefundisha timu mbili tofauti na zote amezipa mafanikio, ameipa Ubingwa Simba Queens, amekuja Simba Senior Team, Simba SC inaelekea kupigania nafasi mbili za juu na zenye thamani kwenye Ligi yetu. Kwani asiwe Kocha Bora?
Waambieni watu Juma Mgunda ndio Kocha Bora msimu huu, kama unabisha mchukuwe Kocha wako, mpe timu ya wanawake kama anaweza kuchukuwa Ubingwa, maana yake huyu mtu ana maarifa mengi sawa na akisa Isaac Newton.
Kusema ukweli anashawishi kumkabidhi jahazi aliendeshe, kwa sababu anaweza na amethibitisha hilo, hii Simba SC ilivyokuwa hohe hahe, Juma Mgunda ameirudisha katika ubora wake, hivi nyinyi hamshtuki? Kwa hiyo hata viongozi wa Simba SC nao watakuwa wanajiuliza nini cha kufanya kwa kocha Mgunda.
Na Juma Mgunda hapigani na waamuzi, ukimuona Mgunda yeye ana furahi muda wote, huyu amefunzwa, sio msela msela, yeye anakukumbusha hebu chezesha kwa haki, sio kwamba hana nguvu, huyu anaheshima na anamuheshimu kila mtu.” Amesema Meneja Habari na Mawasilino Simba SC Ahmed Ally baada ya ushidi wa 3-0 dhidi ya Azam FC