Boniface Gideon – Tanga.

Ujenzi wa Barabara za Maramba Wilayani Mkinga ili kuunganisha na ile ya Mashewa Korogwe hadi Old Korogwe, Barabara ya Handeni-Kilindi, Handeni-Turiani na Barabara ya Mkata-Kwamsisi, zimeanza kunukia lami huku ujenzi wa Barabara Tanga Jiji-Pangani ukifikia asilimia 74 na Daraja la Mto Pangani, likifikia asilimia 25 ambapo zaidi ya Bil.294 zinaendelea kutumika.

Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini – TANROADS, Mkoa wa Tanga, Mhandisi Dastan Singano amewaambia Waandishi wa Habari kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kuunganisha Mtandao wa Barabara mkoani Tanga, ili kufikia lengo la Serikali la kuhakikisha Barabara zote zinapitika wakati wote.

Amesema, “tunaendelea kuunganisha Mtandao wa Barabara kwakiwango cha Lami na Changarawe, kwasasa Barabara zote za Mkoa wa Tanga zinapitika wakati wowote na tunashukuru hatujapata madhara Makubwa za mvua za hivi karibuni ikiwemo kimbunga Hidaya.”

Akizungumzia Mtandao wa Barabara Mkoa wa Tanga kwa kiwango cha Lami, Singano amesema zipo Barabara ambazo ujenzi wake kwakiwango cha Lami unaendelea ikiwemo Tanga Jiji-Pangani lakini pia zipo Barabara ambazo zimeingia kwenye utaratibu na zitajengwa kwakiwango cha Lami,hii ni baada ya Barabara hizo kufanyiwa upembuzi yakinifu.

“Barabara za Handeni-Mafuleta, Handeni-Turiani,Soni-Bumbuli kupitia Dindila hadi Kwameta Korogwe, Barabara ya Tanga-Maramba kupitia Mashewa -Kwamkolo Hadi Old Korogwe Km.127 hizi zote zipo kwenye mpango wa Serikali, lakini pia tuna mtandao mkubwa wa Barabara za Changarawe nazo zote zinapitika wakati wowote” Amesema Singano

kuhusu wizi wa Alama za Barabarani, Singano, amesema “Barabara ya Mkata-Handeni imeibiwa alama za Barabarani kwakiwango kikubwa zaidi kuliko Barabara zote za Mkoa wa Tanga, niwaombe Wananchi kila mmoja awe mlinzi wa Barabara zetu,kwani Serikali inatumia gharama kubwa kufanya Ujenzi wa Barabara zetu hivyo ni vyema kila mmoja wetu akawa ni mlinzi wa mwenzake.”

Pinda: Wakulima wakisimamiwa vizuri watamudu maisha
Putin afanya mabadiliko safu ya ulinzi