Aliyewahi kuwa Mkaguzi wa Chakula cha Rais, Mzee Abdallah Chasamba amesema nguvu nyingi alizojaaliwa na Mwenye enzi MUNGU zilimsaidia kuwa karibu na Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere, wakati walipokuwa wakiendesha harakati za kudai uhuru kutoka kwa Wakoloni.

Mzee Chasamba aliyasema hayo katika mahojiano maalum na Dar24 Media nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa alijaaliwa nguvu nyingi na Mwenye enzi MUNGU na kwamba hilo ndilo lilimsaidia kupata ajira kipindi hicho na kumudu maisha.

Amesema, kutokana na nguvu zake hizo, Mwl. Nyerere alimpa jina la Kamanda kwa jinsi alivyoweza kumshughulikia mtu mmoja aliyekaidi utaratibu uliowekwa, wa kutopita eneo la nyumba ya Baba wa Taifa baada ya saa moja usiku.

“Mwalimu alikuwa amejipumzisha, na sisi tulikuwa tunalinda ila tumebandika tangazo kuwa hairuhusiwi mtu kupita baada ya jioni jirani na nyumba ya Mwalimu pale Magomeni, kipindi hicho anadai uhuru na ameanzisha Chama cha TAA, sasa kuna kijana sijui kwa akili zake au alitumwa akapita eneo lile nilimzuia kwa sauti hakusikia,” alisema Chasamba.

Amesema, “akawa anauuliza kwanini tunazuia watu kupita ndipo nikamnyayua kichwa chini miguu juu, akaanza kupiga kelele kumbe Mwalimu Nyerere akaniona akiwa juu ghorofani, akacheka na kuniita akisema ‘Mzee muache basi inatosha,’ nami nikamtupia huko yule kijana basi kuanzia siku hiyo Nyerere akawa ananiita Kamanda,” alisimulia Mzee Chasamba.

Young Africans kutangaza ubingwa leo?
Pinda: Wakulima wakisimamiwa vizuri watamudu maisha