Kocha Mkuu wa Tottenham Ange Postecoglou amesema amejifunza mambo mengi yaliyokuwa yakiizungumka klabu hiyo kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Man City, uliopigwa usiku wa jana Jumanne (Mei 14), katika Uwanja wa Tottenham jijini London.

Spurs ilipoteza mchezo huo kwa kukubalia kufungwa 2-0 na kuipa nafasi kubwa Manchester City kutetea Ubingwa wao, huku Arsenal wakisubiri hadi michezo ya mwisho ya msimu huu itakaopigwa Jumapili (Mei 19).

Kocha Postecoglou amesema saa 48 zilizopita ambazo zilizunguka pambano la Tottenham dhidi ya Manchester City zimemfunulia misingi tete ndani na nje ya klabu hiyo, ambayo alianza kuifundisha mwanzoni mwa msimu huu 2023/24.

Meneja huyo mzaliwa wa Nea Filadelfeia, Athens, Ugiuriki lakini anatambulika kama raia wa Australia, amesema alichukizwa sana na hali ya ndani ya Uwanja wa Tottenham Hotspur.

“Saa 48 zilizopita zimenidhihirishia kwamba misingi ya klabu hii ni dhaifu. Hicho ndichi nilichokiona. Nje na ndani. Kila mahali. Limekuwa zoezi la kuvutia lakini limekera sana.

“Saa 48 zilizopita zimenidhihirishia kidogo na hiyo si sawa, hiyo inamaanisha kwamba lazima nirudi kwenye ubao wa kuchora kwenye baadhi ya mambo, ili kuweka mambo sawa bila kujali itikadi zetu wala za majirani.”

Postecoglou ameongeza: “Pengine nilisoma vibaya hali hiyo juu ya kile ninachofikiria ni muhimu katika jitihada zetu za kuwa timu ya ushindi lakini hiyo ni sawa, ndiyo sababu niko hapa.”

Mechi ya kuelekea pambano la Spurs ilizingirwa na mjadala kati ya mashabiki wa klabu hiyo ambao walizua mzozo, ambapo baadhi yao walikuwa tayari kuona timu yao inapoteza ili kuinyima nafasi ya Ubingwa Arsenal ambayo ni mshindani wao mkubwa kutoka Kaskazini mwa London na wengine walitamani kushinda mchezo huo.

Endapo Spurs ingechomoza na ushindi dhidi ya Man City ingekuwa na matumaini makubwa ya kuwa sehemu ya timu kutoka England zitakazoshiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao, wakati huohuo wangeipa nafasi Arsenal katika mbio za ubingwa.

Kama Spurs wangeshinda, Arsenal ingesalia pointi moja mbele ya City kileleni mwa Msimamo wa Ligi ya Kuu ya England, huku mchezo mmoja ukisalia.

Mateso: Rais, wanawe wawili wagoma kula
Madai ya vipigo, adhabu kisa ushuru, Mchengerwa atoa tamko