Keshokutwa Jumamosi (Mei 18) Usyk atapigana na Bondia Tyson Fury kwenye pambano la ubingwa wa dunia linalotambuliwa na WBC, WBO, WBA na IBE.

Pambano hilo la uzito wa juu litakalooneshwa mbashara kwenye kituo cha runinga cha Skysport, litaamua bingwa wa uzito wa juu duniani.

Bondia huyo kutoka Ukraine kama atashinda pambano hilo atakuwa bingwa wa uzito tofauti baada ya awali kushinda mataji yote ya uzito mwepesi.

Usyk alikuwa bingwa wa dunia wa mataji yote yaliyounganishwa kwa kumpiga Anthony Joshua lakini pambano hili kwa Fury linawakilisha wakati muhimu kwake kwenye maisha ya mchezo wa ngumi.

“Ninakusanya nguvu zangu kwa sababu Jumamosi ni siku muhimu sana kwangu,”

“Watu wengi wanaofundisha ngumi na waliokuwa na nafasi ya kupigana uzito wa juu, watu wote walikuwa na ndoto za kuingia kwenye uzito wa juu. Ni hatua kubwa, ni mfalme kwenye mchezo wa ngumi.” amesema Fury

Serukamba azionya Taasisi zisizotumia mfumo wa NeST
RC Sendiga: RUWASA endeleeni kutoa huduma bora kwa Wananchi