Aliyekuwa Rais wa Gabon, Ali Bongo na wanawe wawili, Jalil na Bilal wamegoma kula wakilalamikia madai ya kufanyiwa vitendo vya mateso na ukatili wakiwa kizuizini.

Bongo ambaye alifanyiwa mapinduzi ya kijeshi Agosti 2023 ikiwa ni muda mfupi baada ya kushinda kura ya urais iliyoleta mzozo alizuiliwa nyumbani kwake katika mji mkuu, Libreville, pamoja na wanawe hao wawili.

Mawakili wa familia hiyo, wanasema tayari wamewasilisha malalamiko katika Mahakama ya Paris, wiki moja kabla ya Kiongozi wa Serikali ya Gabon, Brice Oligui Nguema kuzuru Ufaransa.

Bongo (64) aliongoza nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu 2009 alipomrithi baba yake ambaye alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 40.

Jaji Mwambegele: Ongezeko la wapiga kura asilimia 18.7
Postecoglou: Saa 48 zimenifunza mengi