Klabu ya Chelsea iko tayari kumuuza Trevoh Chalobah kwa Pauni Milioni 25 msimu huu wa joto na inapania kutoa ofa kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 24.
Kwa mujibu wa Gazeti la Telegraph, Mchezaji huyo kutoka England alitakiwa na Tottenham, Bayern Munich na Nottingham Forest msimu uliopita wa joto.
Pendekezo la kwanza kwa beki huyo ni kucheza soka lake nchini England na kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu yoyote atakayoitumikia.
Gazeti la Telegraph limeandika: “Uhamisho wa kwenda Bayern ulishindikana mwishoni mwa dirisha la usajili la majira ya joto lililopita na Miamba hiyo ya Ujerumani ikamsajili Eric Dier, wakati Tottenham bado wanataka kusajili beki mpya wa kati.
“Inaaminika kuwa Chelsea imemthaminisha Chalobah kwa takriban Pauni Milioni 25 katika kipindi hiki cha majira ya joto na uhamisho wake utasaidia Kanuani ya matumizi ya fedha ‘FFP’.
“Majeraha yalikuwa sababu kwa Chalobah hacheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza msimu wa 2023/24. Alirejea kikosini mwezi Februari na amefanya vyema, na Chelsea haikupoteza mchezo hata mmoja wa Ligi ambayo alianza.
“Chalobah ilianza mechi zote tano za mwisho za Ligi ya Chelsea ambayo walishinda ili kupata kufuzu kwa Uropa kwa msimu ujao na kufunga katika ushindi dhidi ya Tottenham kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.”