Kocha Mkuu wa Kikosi cha Tottenham Ange Postecoglou ameushinikiza Uongozi wa klabu hiyo kuhakikisha unafanya usajili wa wachezaji angalau watatu wapya, ambao wataongeza nguvu kwenye kikosi chake msimu ujao 2024/25.

Kocha huyo raia wa Australia, yuko katika hali mbaya baada ya kumalizika kwa msimu akiwa katika mazingira magumu, kuafutia kikosi chake kufanya hovyo kwenye michezo ya mwisho ya msimu wa 2023/24 uliofikia tamati Jumapili (Mei 19).

Postecoglou anaamini kuwa Spurs ina kila sababu za kuhakikisha kikosi chake kinakuwa imara, hivyo amewataka viongozi wake kuhakikisha mpango huo unafanikiwa katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya joto.

Kwa mujibu wa Televisheni ya ESPN, Kocha huyo anahitaji wachezaji wenye hadhi kubwa, ambao wataleta ushindani wa kweli dhidi ya wachezaji aliowakuta klabuni hapo.

Hata hivyo ESPN imeongeza kuwa, Uongozi wa Spurs huenda ukamtimizia Kocha Postecoglou ombi lake, kwani unatarajia kuuza baadhi ya wachezaji klabuni hapo katika kipindi hiki cha usajili.

Spurs walimaliza katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England msimu wa 2023/24 nyuma ya Aston Villa, na kupoteza nafasi ya kushiriki Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao 2024/25.

Mwamba ameikacha Rayo Vallecano
Awamu ya kwanza ya Mbegu yawasili Rufiji