Mlinda Lango wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City Ederson Santana de Moraes anatajwa kuwa mbioni kuihama klabu hiyo, iliyomsajili miaka saba iliyopita.
Taarifa zilizochapishwa kwenye Gazeti la The Mirror mapema leo Jumatano (Mei 22), imeeleza kuwa Mlinda lango huyo kutoka nchini Brazil anajipanga kuondoka na kutimkia Saudi Arabia.
Ederson mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na City kutoka Benfica mwaka wa 2017, na kushinda mataji Sita ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Makombe mawili ya FA.
Gazeti hilo limeandika: “Ederson anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wa hadhi ya juu zaidi kuondoka kwenye kikosi cha Pep Guardiola katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Mashabiki wa Man City wanahofia huenda Mlinda Lango huyo chaguo la kwanza akawa tayari kuondoka baada ya miaka saba klabuni hapo, huku Ligi Kuu ya Saudia ikitajwa kumtwaa.
“Ingawa Man City hawataki kumwachia Ederson, lakini endapo itapokea ofa kubwa huenda ikamruhusu.”