Waandishi wa Habari Nchini, wametakiwa kuendelea kuhabarisha umma juu ya mafunzo ya usalama na afya mahala pa kazi, kwani wao ni kikuu cha kuwaunganisha Wananchi na Serikali ambayo huona na kusikia, kisha kufanyia kazi yale yote yanayoonekana ni changamoto kwa jamii .
Akizungumza hii leo Mei 22, Jijini Dodoma katika mafunzo yaliyotolewa na OSHA kwa Waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema Waandishi wa habari ni watu pekee ambao ndio chanzo kikubwa cha kuhabarisha umma na kuwafikia watu wengi.
Amesema, “kuna makundi mengi kupitia ninyi najua mtaenda kuhabarisha umma masuala ya usala na afya mahali pa kazi, ili kuendelea kuwa kwenye ajira ni lazima uwe na afya njema na mazingira makubwa ya kazi yanayo muathiri mfanyakazi ni kuaribika kisaikolojia.”
Hata hivyo, amesema na nguvu kazi yote ya OSHA ni ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba uwepo wa taasisi hiyo ni utashi wa serikali ambayo imeona Mwanandamu ana thamani hivyo kuwekeza kwa kutoia vifaa vifaa vya kisasa, na mazingira ya kazi kuwa rafiki.