Katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali madini, mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yametoa fursa ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini, ambapo suala la ushirikishwaji wa wazawa limepewa kipaumbele, ili kuhakikisha wazalishaji na biashara ya Madini zinatoa kipaumbele kwa Watanzania. .

Hayo yamesemwa leo Mei 22, 2024 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde katika ufunguzi wa Jukwaa la Tatu la Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini linaloendelea kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano AICC, jijini Arusha.

Amesema, “marekebisho ya mwaka 2017 ya Sheria ya Madini, yalipelekea kutungwa kwa Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania za Mwaka 2018 ili kuweka usimamizi thabiti katika utekelezaji wa masuala ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini nchini.”

Mavunde ameongeza kuwa, “kulikuwa na malalamiko mengi, watanzania walikuwa ndugu watazamaji mpaka vyakula vilikuwa vinatoka nje, lakini baada ya mabadiliko ya sheria ya mwaka 2017 ushirikishwaji wa watanzania umekuwa mkubwa sana sambamba na watanzania kushika nafasi za juu za uongozi kwenye kampuni za madini.”

Aidha, amesema katika kipindi cha Julai, 2023 hadi Machi, 2024, Wizara kupitia Tume ya Madini ilipokea na kupitia jumla ya mipango 801 ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika shughuli za Madini sawa na ongezeko la asilimia 57 ikilinganishwa na mipango 510 iliyopokelewa katika kipindi kama hicho kwa Mwaka wa Fedha uliopita.

Hata hivyo amesema, mauzo hayo yaliyofanywa na kampuni za kitanzania kwa mwaka 2023 yalikuwa ni zaidi ya mauzo yaliyofanywa mwaka 2022 ambayo yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.08 sawa na asilimia 86 ya mauzo yote ya Dola za Marekani bilioni 1.26.

Habarisheni umma usalama, afya mahala pa kazi - Mwenda
Dkt. Mzuri: Maadhimisho uhuru wa Habari yatagusia sheria rafiki