Beki kutoka DR Congo Henock Inonga Baka amefunguka kuhusu sakata lake na Simba SC ambalo limechukua majuma kadhaa, huku akiwa haonekani kikosini kwa sasa.

Inonga mara ya mwisho alionekana kwenye kikosi cha Simba SC wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans uliomalizika kwa Miamba ya Jangwani kuibuka na ushindi wa 2-1, Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa amekiri yupo nchini Ufaransa kwa mapumziko, akiamini siku kadhaa zijazo atakuwa anamalizana na Simba SC kwa mujibu wa mkataba uliokuwa unamuweka klabuni hapo.

Inonga amesema hadi sasa anachofahamu ana mkataba na Klabu hiyo ya Msimbazi hadi mwishoni mwa msimu huu, licha ya taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi kudai bado ana mkataba wa mwaka mmoja zaidi.

Hata hivyo amedia kuwa suala la sakata lake la kimkataba na Simba SC kwa sasa lipo chini ya Mwanasherai wake na ana uhakika litamalizwa kisheria.

“Mimi siujui huo mkataba wanaousema wao mimi navyofahamu ni kwamba Mkataba wangu unamalizika msimu huu na hivyo ndivyo ilivyo, hili jambo lipo kwa Wanasheria wangu kwa sasa nipo Ufaransa kwa Mapumziko.”

“Ninaimani kubwa sana na Mwanasheria wangu hili suala atalimaliza kisheria na nitakuwa huru kucheza popote, japo kwa sasa ninachokifahamu ni kwamba mkataba wangu utafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.” amesema Inonga

Beki huyo aliyejiunga na Simba SC miaka miatatu iliyopita akitokea Daring Club Motema Pembe ya nchini kwao DR Congo, anahusishwa na Mabingwa wa soka nchini Morocco FAR Rabat wanaonolewa na aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi.

Kilo 110 za Bangi zawaumbua wawili Tanganyika
Ajira: Serikali kuwapa kipaumbele wanaojitolea